DKT. MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI VYETI KWA WATOTO - TSJ WARRIORS

Breaking



Wednesday, September 27, 2017

DKT. MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI VYETI KWA WATOTO



Na. Mwamvita Mussa

Vaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. John Palamagamba amezindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Matogolo Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara ukiwa na lengo la kuwasajili watoto waliochini ya umri miaka mitano pamoja na kuwapatia vyeti ambavyo vitawasaidia kutambulika kwao na kisha kupewa nyaraka za uthibitisho yaani vyeti vya kuzaliwa.
Waziri Mwakyembe amesema kwamba, katika kupanga maendeleo ya nchi kunahitajika takwimu sahihi za matukio muhimu za Watanzania ambazo zinaelezea taarifa zao za kuzaliwa ikiwemo za vifo kwakuwa takwimu hizo zinasaidia kujua mahitaji ya wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, lishe pamoja na sehemu nyinginezo
Mpango huu utaondoa utegemezi wa takwimu za kuhisia, takwimu za kukadilia ndugu zangu mfumo tulionao sasa unategemea Sensa ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10, na matukio bado yanatokea, hivyo kutumia Mpango huu kutasaidia kupata takwimu sahihi na halisi za Watanzania wote”, alisema, Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, Mikoa ya Lindi na Mtwara itanufaika na mpango huo kwakuwa Serikali itakuwa inatambua mahitaji halisi ya wananchi kupitia taarifa zitakazochukuliwa za uandikishaji wa watoto hao, huku akisisitiza kuwa, anaamini kwamba mikoa hiyo itakuwa chachu ya kuongezeka kwa idadi ya watoto watakaoandikishwa kama ilivyofanyika katika baadhi ya mikoa mingine ya Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome amesema kwamba kama Wizara wana wajibu wa kufikisha huduma hiyo kwa wananchi hususani kwa wananchi ambao wako maeneo ya mbalibila kujali hali yao ya kimaisha huku akisisitiza kwamba kila mtoto atapatiwa haki hiyo ya kuandikishwa na kupewa cheti hivyo.
“Kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano ana haki ya Kikatiba ya kupewa huduma hii, hivyo tutahakikisha kwamba kila mtoto katika Taifa letu anapewa huduma hii bure kupitia RITA”, alisema Prof. Mchome

No comments:

Post a Comment


Pages