WAZIRI WA NISHATI AISHUKIA TANESCO, 'HATUWEZI KUIWEKA NCHI GIZANI KWASAA 10’ - TSJ WARRIORS

Breaking



Thursday, October 26, 2017

WAZIRI WA NISHATI AISHUKIA TANESCO, 'HATUWEZI KUIWEKA NCHI GIZANI KWASAA 10’

Na. Joseph Abel
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameonyesha kutoridhishwa na baaadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Nchi hali iliyopelekea umeme kukatika hapo jana eneo kubwa la nchi na kuwataka kuandika barua za kujiuzulu endapo hali hiyo itaendelea.
Waliotakiwa kufanya hivyo ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa uzalishaji Abdalla Ikwasa, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa usafirishaji Tanesco  Mhandisi Bishaija Kahitwa na Meneja udhibiti mitambo wa Tanesco Isihaka Mosha,
“Hatuwezi kufanya kazi kwa mazoea, hatuwezi kuweka nchi gizani kwa masaa 10, nadhani tumeelewana na hapa hakuna maswali nataka kila mtu achape kazi kwa nafasi yake, huwezi ondoka, hao wawili nimeshaambia leo umeme ukizimika nikute barua wameshajiuzulu” amesema Dkt. Kalemani.
Uamuzi huo unakuja baada ya kutoridhishwa na taarifa ya kukosekana kwa umeme kote nchini ambapo ameagiza Meneja wa kituo cha kufua umeme cha Kidatu aondolewe mara moja.

No comments:

Post a Comment


Pages