MAVAZI BADO NI JANGA LA TAIFA - TSJ WARRIORS

Breaking



Wednesday, September 27, 2017

MAVAZI BADO NI JANGA LA TAIFA


Na. Mary Mafuru
Image result for fashion za ushonaji
Kimsingi,tafsiri ya mavazi ya heshima ni Yale yanayozingatia mila na desturi ya Jamii husika, mavazi ni moja ya utambulisho katika Jamii, kabila na hata makundi mbalimbali katika Jamii na ndio maana ya maneno kama vazi la taifa,vazi la michezo,sare za mahitaji mbalimbali na hata kuna baadhi ya watu hujiwekea utambulisho binafsi kupitia mavazi.

Uzuri au ubaya wa kitu unatafsiri mbalimbali ambazo zinafanya nafsi ya mtu kujieleza ,mara nyingi mavazi katika namna ya kipekee Yana nafasi kubwa zaidi ya kuwasilisha ujumbe.

Pamoja na uzuri wa kitu au mambo,unaopatikana kupitia mavazi,katika sura ya pili matumizi mabaya au upotoshaji wa namna yoyote katika  matumizi yake ,yamezua matatizo makubwa katika Jamii, hata kufarakanisha  wanafamilia.

Sasa malalamiko yametawala,kiasi cha kwamba hata wenye nyumba za ibada ambako kunaheshimiwa kwa namna ya kipekee,matumizi mabaya ya mavazi moja kwa moja huwasilisha ujumbe wa kutoheshimu sehemu hizo.

Vazi linaloendana na mahitaji ya miongozo ya ngazi husika,Yana maana kubwa sana.
Mathalani,katika sehemu nyingi staha ya mwanadamu ni kuvaa nguo inayohifadhi baadhi ya sehemu za maungo ya miili yao,ambayo kwa mujibu wa imani na desturi si mahali pa kuachwa wazi.

Kwa kutumia kigezo hicho ndiyo inazaa marufuku kwa baadhi ya mavazi ama yasivaliwe kabisa au hayapaswi  kuvaliwa katika baadhi ya mazingira na maeneo mfano hai ukiwa ni kutoruhusu mavazi ya michezo kuvaliwa na wafanyakazi katika sehemu wanakotumikia.

Tafsiri hiyo inaenda mbali zaidi kwa kina mama kuambiwa mavazi yanayobana,fupi kuacha magoti na sehemu za mwili wazi,hali kadhalika kitovu na kifua.

Mwaka 1971,Chama cha TANU ambacho kilikuwa kimeshika hatamu za uongozi wananchi wakati huo  kilitoa waraka maalumu wenye mwongozo kuhusu mavazi .

Madhumuni ya waraka huo,yalikuwa kuimarisha heshima ya taifa,kwa mujibu wa imani ya Jamii yake,ikilenga kuhakikisha kuwa watumishi katika sehemu za kazi wanadumisha staha ya  heshima wawapo kazini.

Tukichukua kinachojiri leo mbele ya umma kuhusu mavazi na kikichoagizwa kwenye waraka huo wa TANU,tofauti ni ya kutisha. Mitindo ya mavazi hivi sasa inaporomosha thamani ya jinsia zote mbili katika Jamii .kwa kifupi hali ni tete.

Pengine hali ingekuwa ni mbaya zaidi,lakini tunapaswa kuzishukuru asasi za kidini,sehemu ambako imani ya umma imeshikiliwa .
Kwa watoto wa kike, imekuwa sehemu ya maisha yao ya kuvaa nguo fupi zinazoonyesha umbiko la miili yao.

Kwa tafsiri yao,wanajihisi wanakuwa  warembo zaidi na wanakubalika katika Jamii yao ya kitanzania ,kwa kukumbatia utashi huo wenye mzizi
Kwenye utandawazi.

Ni jambo linalowagharimu wengi katika Jamii,baadhi,baadhi wakifukuzwa au kuzuiwa kuingia kwenye maofisi na nyumba za ibada au hata kutokukubalika katika makazi binafsi.Jumuiya ambayo msingi wake ni mkusanyiko wa watu kwa lengo maalumu ina tafsiri Pana,pia huendana na haja ya mtu mmoja mmoja au kikundi kutaka kukubalika nayo.

Inaweza kuwa kwenye kituo cha basi,sokoni,hospitali,nyumba za ibada,mashuleni au vyuoni.
Moja ya tiketi muhimu katika kujumuika nayo ni vazi linalolubalika,kama nguo ndefu kwa kina mama ambayo ina kawaida ya kumbandika a lama ya kimantiki kwa mvaaji ni mstaarabu.
Katika mavazi kuna neno kujisitiri ambalo maana yake ni kuficha kitu mahali ili kisionekane.
Lakini kwa karne ya sasa wanaume kwa wanawake wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na staha kwenye Jamii.

No comments:

Post a Comment


Pages