| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli |
Na. Mary Mafuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli ataka jiji la Arusha liwe jiji la mfano huku akiwataka wananchi kuachana na siasa uchwara
Akizingumza na wananchi wa Sangsi nje kidogo ya jiji la Arusha hapo jana akiwa anaelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) amewataka wananchi wa Arusha kujenga maendeleo yao kwasababu maendeleo hayana Chama.
“nataka Arusha liwe jiji la kweli na ninaomba ndugu zangu wa Arusha achaneni na siasa uchwara endeleeni kujenga maendeleo “Alisema Magufuli.
Aidha Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa waendelee kujenga maendeleo kwasababu hayana uchama na watu waache kuwahubiria na kuwaacha wanahangaika barabarani.
“tunachotakiwa sisi watanzania ni kuleta maendeleo ya kweli bila kubagua vyama,dini na makabila yetu ,mimi kama kiongozi wenu sijabagua”,Alisema Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment