| Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu |
Na Oliver Mathias
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amezuia vibali vya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa mtu yoyote hata Rais wa Nchi.
Aliyasema hayo katika hospitali ya Muhimbili Wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto.
Mwalimu amesisitiza kuwa mgonjwa yoyote anayehitaji kupelekwa nje ya Nchi kwa matibabu lazima apate kibali kwa mganga mkuu wa hospitali ya Muhimbili kwa kukili kuwa mgonjwa ameshindwa kupata matibabu kutokana na sababu maalumu.
Aidha aliendelea kwa kusema “msione aibu kusema kuwa mmeshindwa kumtibu mgonjwa mwisho wa siku akapoteza maisha,isiwe hivyo inaposhindikana mnatoa taarifa”Alisema Mwalimu
No comments:
Post a Comment