“UKATILI SASA BASI” - TSJ WARRIORS

Breaking



Wednesday, September 20, 2017

“UKATILI SASA BASI”



Na. Mwamvita Mussa

 Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake vimekithiri kwa wakazi wa mtaa wa Mafuriko, wilaya ya Ilala jijini Dar es slaam.
       
Akizungumza na mwandishi kutoka TSJ mwenyekiti wa mtaa huo  Bw. Abdallah Twaha amesema kuna takribani  kesi  45 za matendo hayo,  ambapo wanawake wanapigwa na hata kufukuzwa kwenye makazi yao.
      
 Aliendelea kwa kusema kwamba  mfumo dume ndio chachu ya ugomvi katika kaya nyingi kwa sababu mwanamke ametumika kama chombo cha starehe.
       
Vilevile wanawake wengi hawapati furaha katika familia, na wengi wamekuwa wakipigwa, pia wajane wanaonewa kwa kupokonywa mali zao na hata kulazimishwa kurithiwa ikiwa ni mila na desturi.
     
“ mara nyingi alikuwa akirudi usiku na nilipomuuliza alinipiga  na hata kunichana na viwembe, ila ninawashukuru Ustawi wa Jamii kwa msaada wa sheria walionipatia” alisema Faith Mussa mwanamke mhanga katika ukatili wa kijinsia.
      
 Hata hivyo, mtaa wa Mafuriko kwa kushirikiana na wananchi wameandaa mkakati  wa kupambana na vitendo hivyo vya ukatili kwa kuunda timu ya watu sita ambao watahusika katika kutoa elimu kila mwisho wa wiki kwa kuandaa mikutano mbalimbali.
       
Tanzania ina jumla ya mikoa 27 ambapo mkoa wa Shinyanga ndio mkoa unaoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake haswa katika ndoa zaa utotoni na mimba za utotoni,takwimu zinaonesha ni  asilimia 59 ikifuatiwa  na Tabora asilimia 58 na Mara asilimia 55

No comments:

Post a Comment


Pages