MCHEKESHAJI MAARUFU APATA AJALI MBAYA - TSJ WARRIORS

Breaking



Wednesday, September 20, 2017

MCHEKESHAJI MAARUFU APATA AJALI MBAYA




Na.Erick Kelvin
         
     Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili anepata ajali ya gari alipokuwa akitoka Mwanza kuelekea Shinyanga.
           
Kamanda wa  polisi mkoa wa Shinyanga Saimoni Haule amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika kijiji cha Mwanishoni  kata ya Bumiki wilayani Kishapu  na amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi alasiri na kuhusisha  gari binafsi yenye namba  za usajili T 362 BAE Toyota Prado, iliyokuwa na watu watatu dereva aliyejulikana kwa jina la Said Hasani mkazi wa Dar es salaam, kamanda Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitali ya Bugando.
          
 Afisa mahusiano wa hspitali ya Bugando Luki Joseph amethibitisha kupokea majeruhi watatu na miongoni mwa majeruhi hao ni MC Pilipili, amesema kwa sasa wanaendelea vizuri na hali zao zinaewndelea kuimarika.

No comments:

Post a Comment


Pages