TANZANIA KUPIGA VITA UKEKETAJI - TSJ WARRIORS

Breaking



Wednesday, September 20, 2017

TANZANIA KUPIGA VITA UKEKETAJI



Na. Joseph Abel

  Licha ya juhudi nyingi zinazofanywa na serikaali kwa kushirikiana na taasisi binafsi juu ya kudhbiti  vitendo vya ukeketaji lakini bado ni changaamoto kubwa katika jamii nyingi nchini Tanzania.

 Mratibu wa masomo katika chuo cha uandishi wa habari cha TIME School of Journalism (TSJ), Blandina Semaganga amesema kuwa, vitendo hivi ni hatari kwa afya ya binadamu sababu vinaweza kupelekea kifo cha mama hasa pale anapojifungua.

“ hili suala bado makabila mengi wana lipractise na halitakiwi kiafya, sababu limekuwa likileta madhara kwa wanawake hasa wakati wa kujifungua,mama anapofikia wakati wa kujifungua hupoteza damu nyingi na hatimae mtoto anaweza kutoka salama lakini mama akapoteza maisha”.
 Ameendelea kwa kusema, anaishukuru serikali kwa kufanikiwa kupunguza vitendo hivi vya ukeketaji “ lakini kwa asilimia kubwa tunaishukuru serikali kwa kupiga vita suala hili, tunaona linapotea taratibu ila sisemi kama limeisha lakini bado kuna makabila wanafanya vitendo hivi” amesema Semaganga.
    
 Na kwa upande wake mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha (TSJ)  Rodney Malongo amesema kuwa vitendo hivi vinapelekea kuenea kwa maambukizi ya magonjwa sababu kifaa kinachotumika ni kimoja.

“sababu nyingine ni kuenea kwa magonjwa kwa sababu  chombo  kinachotumika kufanya huo ukatili  ni hikohiko kimoja kinazunguka kwa wanawake wengi” amesema mwanafunzi huyo
       
 Aidha amesema Semaganga “ watanzania wote tunatakiwa kujali afya ya kila mmoja hasa afya ya mama, kwani mama ndio mlezi wa familia” amesema.


No comments:

Post a Comment


Pages